(ABNA24.com) Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia mashinikizo ya maadui dhidi ya taifa la Iran na kusisitiza kuwa, nafasi ya taifa kubwa la Iran imekuwa kubwa zaidi kuliko huko nyuma baada ya mwaka mmoja na nusu wa mashinikizo na vikwazo vya mfululizo vya kiuchumi vya maadui.
Rais Rouhani amesema hayo leo (Jumatano) katika kikao cha Baraza la Mawaziri hapa Tehran na kuongeza kuwa, Marekani imeiwekea Iran mashinikizo makubwa sana ya kiuchumi kama vile vikwazo, kujaribu kuvuruga uuzaji mafuta ya Iran na kukwamisha shughuli za benki na bima.
Amesema lengo hasa la Marekani ni kutoa pigo kwa Iran lakini imeshindwa kufikia lengo hilo. Ameongeza kuwa, utulivu katika uchumi wa Iran umekuwa mkubwa zaidi kwenye kipindi cha mwaka mmoja uliopita na kufafanua kwa kusema: Kwa mujibu wa ripoti ya Benki Kuu ya Iran, thamani ya sarafu ya Iran imeongezeka kwa asilimia 40 ikilinganishwa na mwaka jana.
Rais Rouhani amegusia pia safari yake mjini New York Marekani alikokwenda kushiriki kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kuongeza kuwa, kama usingelikuwepo muqawama wa taifa la Iran na utulivu wa kiuchumi pamoja na nguvu za majeshi ya Iran, (Wamarekani) wasingelipanga foleni nje ya chumba cha Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Amesisitiza kuwa, lobi za maadui wa Iran zilikuwa zimeandaa njama maalumu ya kujaribu kuwaambia walimwengu kwamba Iran ndiyo iliyoanzisha vurugu katika eneo nyeti la Ghuba ya Uajemi, lakini nguvu za kisiplomasia za Iran zimesambaratisha njama hiyo.
Amesisitiza pia kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni dola lenye nguvu kubwa katika eneo hili na kwamba kuitenga Tehran ni jambo lisilowezekana kabisa.
/129
Rais Rouhani: Nguvu za taifa la Iran zimeongezeka sana hivi sasa licha ya mashinikizo makubwa ya maadui
3 Oktoba 2019 - 07:16
Msimbo wa Habari: 980098
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia mashinikizo ya maadui dhidi ya taifa la Iran na kusisitiza kuwa, nafasi ya taifa kubwa la Iran imekuwa kubwa zaidi kuliko huko nyuma baada ya mwaka mmoja na nusu wa mashinikizo na vikwazo vya mfululizo vya kiuchumi vya maadui.